Jumamosi, 14 Mei 2016

12310644_787011891409034_7987793355869002041_n (1)
Bomby Johnson ni miongoni mwa wanamuziki ambao wanaaminika kuwa kwa siku za hivi karibuni wataitangaza vyema Tanzania  kupitia Muziki wa injili.Bomby ambaye anajulikana sana kwa wimbo wake “HAKUNA JAMBO LISILOWEZEKANA”  na katika Live Recording ya DVD ya JOHN LISU ali’play part kubwa kama Back up Vocalist wa John Lisu.Jumapili ya leo 8.5.2016 ameiambia YES TANZANIA TV kuwa yuko katika hatua za mwisho mwisho ili kukamilisha album yake mpya.
Bomby ni wanamuziki anayefanya vyema sana kwenye Live Music amesema kwa kuanzia ataachia EP(Extended Play)nyimbo tangulizi nne kati ya nyimbo zinazounda album yake hii mpya.Bomby alizitaja nyimbo hizo kuwa ni
Naamini
Umeinuliwa
Sifa za mioyo yetu
The King of Glory
Kwa upande wa production Bomby amesema album yake hii sehemu kubwa amefanyia  kwenye studio za Push Up Records iliyoko Mbezi beach eneo la Mbuyuni.Push Up Records iko chini ya mtayarishaji mashuhuri Innocent Mujwahuki, kwa ambao hawamfahamu Mujwahuki ama Kanye, ni producer aliyetengeneza 80% ya album ya Angel Benard iitwayo New Day.Tofauti na Mujwahuki Bomby pia amefanya kazi PNEUMA  REC chini ya Producer Baraka ESABU.
john1
Bomby On Stage
Kwa upande wa Video Bomby amesema anategemea Kufanya Live Recording ya album yake hiyo ingawa kabla ya hapo atafanya Video mbili ambazo sio Live.YES TANZANIA TV ilitaka kujua kama yuko chini ya Lebel au management yeyote na Bomby alisema kwa sasa hayuko chini ya Lebel yeyote bali kuna watu anaofanya nao kazi kwa ukaribu sana wakiwepo Push Up Records iliyo chini ya Push Up Entertainment. Let’s wait for Bomby na album yake hii mpya,Hosanna Kwanza tunamtakia kila la Heri katika kazi ya Bwana.
bomby johnson
Bomby The Worshiper

Jumamosi, 26 Machi 2016

All the way from 254 (Kenya), Mr. Seed pamoja Pitson wametusogezea video hii hapa inaitwa "Happy Day". Enjoy!
Tazama video mpya "What God Can Do" all the way from 254 (Kenya) ya kwake Mercy Masika And Liz Gathoni.

Barikiwa na video mpya WATAWALA kutoka kwa mwanamuziki wa nyimbo za Injili Tanzania FRIDA FELIX. Enjoy! 

Jumatatu, 14 Machi 2016


Unaukumbuka huu wimbo 'I Know Who I am' toka kwa mwanadada Sinach? Tazama video hapa chini. Enjoy.
 

Alhamisi, 10 Machi 2016

Hii hapa video nyingine toka kwa Gloria Muliro inaitwa "Ndio Yako" Enjoy!
Tazama video "Nikupendeze" all the way from 255 (Kenya) toka kwa Mwanadada Mercy Masika. Enjoy!
Mtangazaji mahiri wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM Millard Ayo baada ya kufungua studio yake kubwa naya kisasa jijini Dar, ameanza kuuza vipindi vya burudani katika radio mbalimbali za Afrika Mashariki.


Akizungumza Jumamosi hii katika mdahalo wa kuwatia moyo wanafunzi waliofeli kidato cha nne, ambao ulienda sambamba na uzinduzi wa video mpya ya Mrisho Mpoto, Millard alieleza mafanikio yake baada ya kupambana kwa muda mrefu.

“Nilijiuliza kwanini nisitumie uandishi wangu wa habari ili kusambaza habari Afrika?, ndipo nikaanza kujinyima ili nijenge studio yangu kwa pesa yangu mpaka imekamilika. Sasa hivi tayari nimeshaanza kuuza vipindi vyangu katika radio mbalimbali za Afrika, Kenya, Rwanda. 

Pia nimekuwa reporter wa radio mbalimbali za Afrika Mashariki, pia Nigeria kuna kazi maalum nimepata ambayo nimehifurahia sana,” alisema Millard.

Pia Millard Ayo alisema yeye ni miongoni mwa wanafunzi ambao walifeli kidato cha nne lakini aliinuka na kuendelea.

Jumanne, 16 Februari 2016

Ukiacha mashamba, nyumba, magari, Emmanuel Mgaya a.k.a Masanja Mkandamizaji amezindua Mgahawa wake wa Kisasa unaoitwa "Masanja Wali Nyama" Maeneo Ya Tabata Magengeni Karibu na CRDB BANK. 

Shughuli hiyo iliyo anza saa mbili usiku na kumalizika saa tano usiku, ilipambwa na waimbaji mbalimbali wa muziki wa Gospel akiwemo Miriam Jackson, Emmanuel Mbasha, Faraja Ntaboba, Mc Makondeko, Stella Joel pamoja na Wachungaji, Mitume na Manabii. 

Twende sawa na matukio ya Picha hapa chini.

Jumatatu, 15 Februari 2016


Jumapili, 14 Februari 2016

Verse Of The Day
1st John 4:18-19
"There is no fear in love. But perfect love drives out fear, because fear has to do with punishment. The one who fears is not made perfect in love. We love because loved us first." ‪#YESTV(WIMBILAFURAHA)



Nimekusogezea video mpya toka kwa Miriam Jackson inaitwa "Anaweza". Enjoy!

Ijumaa, 12 Februari 2016

HAYAWI hayawi , hatimaye yametimia , YES TV On Air Now Na Mtangazaji wako Hezron Mwanafunzi Wa Yesu tukutane kesho Live kuanzia saa 4:00, lakini bilakusahau jumapili usikose kutazama CHOMOZA YA CLOUDS TV tumewaandalia bonge la zawadi usikose, kutazama TV yako kuanzia saa 1 hadi Saa 4 Asubuhi.




Mkali wa muziki wa injili hapa Tanzania, mwanadada Christina Shusho amekuletea video Mpya inaitwa "MAVUNO".  akishirikiana na Mireille Basirwa, imeandaliwa  Director Tiger kutoka +254
Enjoy! 
 


Alhamisi, 11 Februari 2016

Boni Mwaitege is a dedicated praise and worship servant of God who is using songs to spread the Gospel across the world. His songs has impacted many not only in East Africa but also across Africa and World at Large. Let's pray for this humble servant of God to continue with the mission of service until Jesus returns. When God lifts you up don't despise those who are still down /abusing the favor .The journey is
 
Breath of God we need a touch from You, Shine down on us with the light of truth, Stir our hearts and set our spirit free... Holy Spirit, come fill this place.
 

Jumatano, 10 Februari 2016





 Wakali wa muziki wa injili, Bi. Christina Shusho na Mireille Basirwa wa (Belgium) wamekutana kenya kwa ajili ya kutengeneza wimbo mpya kwenye studio za Produce Timothy Boikwa. Kwa sasa wako Location wakifanya Video ya Kolabo hiyo na Director Tiger.

Tazama picha za utengenezaji wa video hiyo hapo chini.

Machalii wa Yesu kutokea Arusha wamejipanga kuachia wimbo wao mpya unaokwenda kwa jina la Yesu anakupenda ambao uko kwenye mahadhi ya HipHop na umefanywa na vichwa takribani nane vya muziki huo.

Wimbo huo ambao umefanyika chini ya producer Sam Timber kutoka Fnouk studios unatarajiwa kuachiwa siku ya Valentine,tarehe 14/02/2016.

Katika kuelekea kwenye siku ya kuachiliwa kwa wimbo huo, Machalii wa Yesu wanakuletea Yesu anakupenda Challenge ambapo mashabiki na wadau watapewa nafasi ya kuotea hao watu wanane walioshiriki kwenye wimbo huo kwa kuwatambua kutokana na wasifu wa kila mmoja utakaokuwa ukitolewa kwenye ukurasa wa facebook wa Machalii wa Yesu.
 Machalii wamejipanga kuwapongeza watu wa kwanza kuweza kuotea watu hao.

Ungependa kushiriki?Tembelea ukarasa wao wa facebook ambao ni Machalii wa Yesu kisha fuata maelekezo 


Mkali wa muziki wa injili hapa Tanzania, mwanadada Christina Shusho amekuletea video Mpya inaitwa "Unaweza". Enjoy!  

                          Before You End Your Relationship watch this video!
Tazama video toka kenya inaitwa 'Kitanzi' by Willy Paul featuring Gloria Muliro. Enjoy!
      Tazama video 'Mwema' by Mercy Masika toka Nairobi Kenya. Wimbo umeandikwa (tungwa) na Mr.Vee. Enjoy!
This is a VIDEO of MARTHA MWAIPAJA AND HER YOUNG SISTER BEATRICE MWAIPAJA which is called "HIVI NILIVYO" . This Video was Directed by "Jackson Joachim" From IVES ENTERTAINMENT. If you want to do your videos withYES STUDIO contact us 0765177715 or you can email us at yestz.org@gmail.com
Video Mpya Kabisa "Have Your Way" toka kwa mwanadada Angel Benard. Unaweza kudownload wimbo huo kupitia link hii https://mkito.com/song/have-your-way
 


Nimekusogezea video hii toka +254 (Kenya). Willy Paul akiwa na Size 8, Kambua na Gloria Muliro inaitwa "Sijafika" Bado namtafuta Yesu. Enjoy!
 

Video mpya kabisa All the way from 254 inaitwa "Nifunze" toka kwa mwanadada Janet Otieno. "Teach me, Lord, the way of your decrees, that I may follow it to the end. Give me understanding, so that I may keep your law and obey it with all my heart."
 

  Anza weekend yako na video hii "Have Your Way" toka kwa Deitrick Haddon.

                     Video mpya toka kwa mtumishi wa Mungu Abwene Mwasongwe "Mzee Wa Siku"


Download wimbo toka kwa janet otieno na christina shusho "Napokea Kwako"

Lyrics

Maisha magumu sana nimepitia 
Nikajaribu kutafuta msaada sikupata 
Nikaendea wanadamu mwisho wakanidharaume) 
Kumbe msaada wa mwanadamu unatoka kwa Mungu 
Nilijua ya kuwa wenye haki ya kubarikiwa\ 
Kumbe baraka ni haki ya kila mmoja 
Nibebadili wazo langu namwelekea Mungu 
Kwake msaada wangu unapatikana 
Msaada wa mwanadamu ni wa muda mfupi 
Nami zamu yangu wa kubarikiwa ee 

Chorus: 
Wakati huu wa kubarikiwa 
Zamu ni yangu, sasa kupokea(\ 
Nimechoshwa, na shida za dunia 
Napokea kwako, Ee Bwana kwako x2 
Napokea kwako, Yesu napokea kwako 
Napokea kwako, Baba napokea kwako 

Nimeamua kwenda zaidi na zaidi 
Nimejipanga hadi nione matunda yake 
Yale Mungu amewekeza ndani yangu 
Najua Mungu yuko kazini kunikamilisha 
Akisema nimebarikiwa, nimebarikiwa tu 
Hata ukipinga wewe leo mimi nimebarikiwa tu 
Mlima gani kuu sana usioung’oa? 
Jaribu gani gumu sana usiloliweza? 
Chozi gani zito kwako usilolifuta? 
Ombi gani kubwa sana usilolijibu? 

(Chorus)
 

Jumanne, 9 Februari 2016

Ladies and gentlemen, Bahati wa kenya anakukaribisha uitazame video yake mpya inayokwenda kwa jina "Itakuwa Sawa". Enjoy!

Jumatatu, 8 Februari 2016

Video ya Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Miriam Jackson " NI BWANA" inaendelea kufanya vizuri ndani ya Tanzania na East Africa kwa ujumla, Video hiyo iliyotaarishwa na iliyochanganywa sanaa kiufundi zaidi na mtaalishaji wa Gospel Music Video, Tiger from Kenya .Tiger amewahi kutengeneza video za Christiana Shusho , kama "Umenifanya ni Ningare" na zinginezo nyingi tu, Miriam anatarajia pia kuachia wimbo mwingine , Audio na video, Video yake Miriam Jackson inatarajiwa kuwa kali zadi baada ya Director Tiger kufanya kweli kwenye video hiyo, cha kufanya wewe mdau wa Miriam unaweza ukalike page ya facebook ya Miriam Jackson Tz - Ni Bwana ili kupata New updates , na Mungu wa Mbinguni na akuabriki sana. pia unaweza ukatazama video ya "NI BWANA" kupitia link hiii

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Inaendeshwa na Blogger.

Sample text

Random Posts

Social Icons

Followers

Featured Posts

Fashion

Technology

Fashion

Find Us On Facebook

Translate

Editors Picks

Events

Video

Popular Posts

Most Popular

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget