Mtangazaji
mahiri wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM Millard Ayo baada ya
kufungua studio yake kubwa naya kisasa jijini Dar, ameanza kuuza
vipindi vya burudani katika radio mbalimbali za Afrika Mashariki.
Akizungumza
Jumamosi hii katika mdahalo wa kuwatia moyo wanafunzi waliofeli kidato
cha nne, ambao ulienda sambamba na uzinduzi wa video mpya ya Mrisho
Mpoto, Millard alieleza mafanikio yake baada ya kupambana kwa muda
mrefu.
“Nilijiuliza
kwanini nisitumie uandishi wangu wa habari ili kusambaza habari
Afrika?, ndipo nikaanza kujinyima ili nijenge studio yangu kwa pesa
yangu mpaka imekamilika. Sasa hivi tayari nimeshaanza kuuza vipindi
vyangu katika radio mbalimbali za Afrika, Kenya, Rwanda.
Pia
nimekuwa reporter wa radio mbalimbali za Afrika Mashariki, pia Nigeria
kuna kazi maalum nimepata ambayo nimehifurahia sana,” alisema Millard.
Pia Millard Ayo alisema yeye ni miongoni mwa wanafunzi ambao walifeli kidato cha nne lakini aliinuka na kuendelea.
Alhamisi, 10 Machi 2016
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 maoni:
Chapisha Maoni