Machalii
wa Yesu kutokea Arusha wamejipanga kuachia wimbo wao mpya unaokwenda
kwa jina la Yesu anakupenda ambao uko kwenye mahadhi ya HipHop na
umefanywa na vichwa takribani nane vya muziki huo.
Wimbo huo ambao umefanyika chini ya producer Sam Timber kutoka Fnouk studios unatarajiwa kuachiwa siku ya Valentine,tarehe 14/02/2016.
Katika kuelekea kwenye siku ya kuachiliwa kwa wimbo huo, Machalii
wa Yesu wanakuletea Yesu anakupenda Challenge ambapo mashabiki na wadau
watapewa nafasi ya kuotea hao watu wanane walioshiriki kwenye wimbo huo
kwa kuwatambua kutokana na wasifu wa kila mmoja utakaokuwa ukitolewa
kwenye ukurasa wa facebook wa Machalii wa Yesu.
Machalii wamejipanga kuwapongeza watu wa kwanza kuweza kuotea watu hao.
Ungependa kushiriki?Tembelea ukarasa wao wa facebook ambao ni Machalii wa Yesu kisha fuata maelekezo
Jumatano, 10 Februari 2016
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 maoni:
Chapisha Maoni