Jumamosi, 14 Mei 2016

12310644_787011891409034_7987793355869002041_n (1)
Bomby Johnson ni miongoni mwa wanamuziki ambao wanaaminika kuwa kwa siku za hivi karibuni wataitangaza vyema Tanzania  kupitia Muziki wa injili.Bomby ambaye anajulikana sana kwa wimbo wake “HAKUNA JAMBO LISILOWEZEKANA”  na katika Live Recording ya DVD ya JOHN LISU ali’play part kubwa kama Back up Vocalist wa John Lisu.Jumapili ya leo 8.5.2016 ameiambia YES TANZANIA TV kuwa yuko katika hatua za mwisho mwisho ili kukamilisha album yake mpya.
Bomby ni wanamuziki anayefanya vyema sana kwenye Live Music amesema kwa kuanzia ataachia EP(Extended Play)nyimbo tangulizi nne kati ya nyimbo zinazounda album yake hii mpya.Bomby alizitaja nyimbo hizo kuwa ni
Naamini
Umeinuliwa
Sifa za mioyo yetu
The King of Glory
Kwa upande wa production Bomby amesema album yake hii sehemu kubwa amefanyia  kwenye studio za Push Up Records iliyoko Mbezi beach eneo la Mbuyuni.Push Up Records iko chini ya mtayarishaji mashuhuri Innocent Mujwahuki, kwa ambao hawamfahamu Mujwahuki ama Kanye, ni producer aliyetengeneza 80% ya album ya Angel Benard iitwayo New Day.Tofauti na Mujwahuki Bomby pia amefanya kazi PNEUMA  REC chini ya Producer Baraka ESABU.
john1
Bomby On Stage
Kwa upande wa Video Bomby amesema anategemea Kufanya Live Recording ya album yake hiyo ingawa kabla ya hapo atafanya Video mbili ambazo sio Live.YES TANZANIA TV ilitaka kujua kama yuko chini ya Lebel au management yeyote na Bomby alisema kwa sasa hayuko chini ya Lebel yeyote bali kuna watu anaofanya nao kazi kwa ukaribu sana wakiwepo Push Up Records iliyo chini ya Push Up Entertainment. Let’s wait for Bomby na album yake hii mpya,Hosanna Kwanza tunamtakia kila la Heri katika kazi ya Bwana.
bomby johnson
Bomby The Worshiper

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Inaendeshwa na Blogger.

Sample text

Random Posts

Social Icons

Followers

Featured Posts

Fashion

Technology

Fashion

Find Us On Facebook

Translate

Editors Picks

Events

Video

Popular Posts

Most Popular

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget