Bomby Johnson ni miongoni mwa wanamuziki
ambao wanaaminika kuwa kwa siku za hivi karibuni wataitangaza vyema
Tanzania kupitia Muziki wa injili.Bomby ambaye anajulikana sana kwa
wimbo wake “HAKUNA JAMBO LISILOWEZEKANA” na katika Live Recording ya
DVD ya JOHN LISU ali’play part kubwa kama Back up Vocalist wa John
Lisu.Jumapili ya leo 8.5.2016 ameiambia YES TANZANIA TV kuwa yuko katika
hatua za mwisho mwisho ili kukamilisha album yake mpya.
Bomby ni wanamuziki anayefanya vyema sana
kwenye Live Music amesema kwa kuanzia ataachia EP(Extended Play)nyimbo
tangulizi nne kati ya nyimbo zinazounda album yake hii mpya.Bomby
alizitaja nyimbo hizo kuwa ni
Naamini
Umeinuliwa
Sifa za mioyo yetu
The King of Glory
Kwa upande wa production Bomby amesema album yake hii sehemu kubwa amefanyia kwenye studio za Push Up Records
iliyoko Mbezi beach eneo la Mbuyuni.Push Up Records iko chini ya
mtayarishaji mashuhuri Innocent Mujwahuki, kwa ambao hawamfahamu
Mujwahuki ama Kanye, ni producer aliyetengeneza 80% ya album ya Angel Benard iitwayo New Day.Tofauti na Mujwahuki Bomby pia amefanya kazi PNEUMA REC chini ya Producer Baraka ESABU.
Bomby On Stage
Kwa upande wa Video Bomby amesema
anategemea Kufanya Live Recording ya album yake hiyo ingawa kabla ya
hapo atafanya Video mbili ambazo sio Live.YES TANZANIA TV
ilitaka kujua kama yuko chini ya Lebel au management yeyote na Bomby
alisema kwa sasa hayuko chini ya Lebel yeyote bali kuna watu anaofanya
nao kazi kwa ukaribu sana wakiwepo Push Up Records iliyo chini ya Push
Up Entertainment. Let’s wait for Bomby na album yake hii mpya,Hosanna
Kwanza tunamtakia kila la Heri katika kazi ya Bwana.
Bomby The Worshiper